Baada ya Dj Khaled kutokea MTV akitangaza mapenzi yake ya dhati kuhusu nia ya kumuoa Nicki Minaj, mrembo huyu wa Young Money ameonekana Crustacean Restaurant Los Angeles Marekani akiwa na pete ya uchumba kwenye mkono wake wa kushoto wakati alipotoka kula chakula cha jioni na baadhi ya marafiki zake waliosoma pamoja High school.
Unadhani hiyo pete kavishwa na Khaled????!!! Biiig No…. kwa
mujibu wa Necole hii ni pete ambayo inaaminika alivishwa na boyfriend
wake wa longtime kitambo anaitwa Safaree ambae nae amekua akionekana
kavaa pete kama hiyo ya gold ambayo imesababisha watu waamini pia
uwezekano wa ndoa ya siri ya wawili hawa.
Dj Khaled na huu mpango wake wa kutangaza nia ya kumchumbia
Nicki Minaj aliiambia Power 106 kwamba anampenda sana Nicki Minaj kama
ambavyo wanaume wengi wamekua wakivutiwa kumuoa pia, lakini akasisitiza
kama Nicki atakataa kuchumbiwa na yeye… hakutakua na ubaya, bado ni
marafiki…
Namkariri akisema ‘Nicki anaweza kutokua tayari kwa ndoa ila
nitamwambia ninachofeel, hata akisema ndio kwangu au akiniahidi mwakani
nitasubiri tu, sitokata tamaa… nataka watoto’
Rapper Rick Ross ambae ni rafiki wa wote Nicki Minaj na Dj Khaled
ametoa baraka zake kama ni kweli hiyo ndoa ipo na miongoni mwa
aliyoyasema ni uwezekano wa kuwapa gari kama zawadi ya harusi yao, mchek
zaidi kwenye video hapa chini ambapo mpaka anahojiwa hapa alikua
hajaiona video ya Dj Khaled akiomba uchumba kwa Nicki huku akiwa na pete
mkononi.
No comments:
Post a Comment