Wednesday, 17 July 2013

BINTI AMCHINJA BABA YAKE BAADA YA KUBAKWA


Baadhi ya wanakijiji wakiwa wameweka ulinzi mkali kuzuia binti huyo asikamatwe na polisi.

Binti mmoja amekata kichwa cha baba yake na kukitenganisha na kiwiliwili kwa kutumia panga baada ya baba huyo kumbaka kwenye nyumba yao iliyoko katika milima ya Papua New Guinea.

Sasa wakazi wa kijiji hicho wameunda wigo kwa ajili ya kumlinda binti huyo wa miaka 18, wakigoma kumkabidhi kwa polisi sababu wanakubaliana kwamba baba yake huyo 'shetani' alistahili kufa.

Kiongozi wa kanisa moja kijijini hapo, Mchungaji Lucas Kumi anayetokea kijiji cha Rang kilichoko kwenye Milima ya Magharibi, alisema jamii nzima imegoma kuruhusu binti huyo kuhusishwa na uchunguzi wowote rasmi.

"Watu na viongozi katika eneo letu walikwenda na kushuhudia mwili usiokuwa na kichwa wa baba huyo baada ya binti huyo kuripoti tukio hilo kwao na kufafanua kwanini alimuua baba yake," alisema Mchungaji Kumi.

Alieleza kwamba baba huyo, aliyekuwa na umri wa takribani miaka 40, alimbaka binti yake walipokuwa peke yao katika nyumba yao baada ya mama na watoto wengine wawili kutoka kwenye familia hiyo kwenda kuwatembelea jamaa zao usiku huo.

"Baba huyo alikwenda kwenye chumba cha binti yake wakati wa usiku na kumbaka kwa kurudia-rudia.

"Baba huyo alitaka kumbaka tena binti yake wakati wa asubuhi na hapo ndipo binti huyo alipochukua kisu na kukata kabisa kichwa cha baba yake," alisema Mchungaji Kumi.

"Wote tumeafiki kwamba binti huyo yuko huru kuishi katika jamii hii sababu baba huyo alistahili kufa.

"Binti huyo alifanya hicho alichofanya sababu ya kuathirika kisaikolojia na vitendo hivyo vya kishetani vya baba yake, ndio maana tumeafikiana kwamba ataendelea kubaka katika jamii hii."

Alisema wigo wa ulinzi umewekwa kumzunguka binti huyo, ambaye atawekwa mbali na uchunguzi wowote rasmi.

"Jamii pia imekubaliana kutoandaa mazishi yoyote ya kawaida kwa ajili ya baba yake huyo."

Makosa ya ubakaji, mauaji, kuuawa kwa watuhumiwa wa uchawi mna ukahaba yametapakaa kote nchini Papua New Guinea na juhudi za kujaribu kukomesha, serikali hiyo isiyofuata sheria hivi karibuni ilianzisha tena hukumu ya kifo kwa makosa makubwa.

Lakini mwishoni mwa wiki iliripotiwa matokeo ya uchunguzi kuhusu watoto wanaofanya ukahaba, ripoti, ilisema, hilo 'litakufanya ujikunyate.'

Watoto wenye umri wa kati ya miaka 13 na 16, inasemekana, walikuwa wakijiuza kwenye klabu za usiku zilizoko katika mji mkuu, Port Moresby, majumba matano yameripotiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba kwa watoto wenye umri mdogo.

Taasisi tatu zisizo za kiserikali zimetoa ripoti iliyoegemea kwenye mahojiano na watoto wasiopungua 175 wanaojihusisha na biashara ya ngono.

"Ni kweli, binti zetu, na hasa wanafunzi wa kike, wamekuwa wakinunuliwa na kuuzwa kwa ajili ya ngono," alisema mmoja wa wachunguzi.

No comments:

Post a Comment