Amini usiamini, Prezzo hakuyachukulia poa majigambo ya Diamond kabla ya Tamasha la Matumaini. Ni kweli kama tulivyohisi awali kuwa Rapcellency alimind na sasa ametupa bomu jingine kwa Diamond.
Prezzo anadai kuwa anamfahamu sana Diamond kama mtu anayependa kujitafutia jina kupitia wapenzi wake wa zamani.
Jana Prezzo alitweet: All along nlijua kuwa ni kawaida yake kutafuta “KIKI” kutoka kwa ma ex wake hadi nliposoma gazeti anaongea utumbo kunihusu. Now it’s ON.”
Hatuna uhakika ila tunahisi kwa kusema ‘now it’s on’ Prezzo anamaanisha ‘beef’.
Wakati huo huo, leo Prezzo ametupa dongo jingine kwa Diamond kwa kutweet, “looking forward to our meeting next week #MagnaCarta, throw ur Diamonds up #Rapcellency #RocNation in the building,” huku akiweka video inayoonesha jinsi walivyokutana na Jay-Z na kwamba watakutana tena wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment