Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini katika kitabu cha maombolezo ya Msiba wa Jaji Mstaafu, Buxton
Chipeta, aliyefariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Makamu alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini
leo Julai 19, 2013.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu Jaji
Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo
nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19,
2013. Marehemu Chipeta, alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini Dar.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwafariji wafiwa ndugu wa marehemu Jaji Mstaafu, Buxton Chipeta,
wakati alipofika kuhani na kuaga msiba huo, nyumbani kwa marehemu,
Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013. Marehemu Chipeta,
alifariki dunia Julai 16, mwaka huu jijini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya Majaji waliohudhuria msiba huo nyumbani kwa
marehemu Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai, 19, 2013 baada ya
kuhani msiba huo wa Jaji mstaafu Buxton Chipeta.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akijumuika na baadhi ya waombolezaji katika msiba wa marehemu Jaji
Mstaafu, Buxton Chipeta, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu
Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo Julai 19, 2013 kwa ajili ya kuhani
na kuaga msiba huo.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu katika msiba huo leo
No comments:
Post a Comment