Habari zilizotufikia kutoka mjini Mtwara Zinasema kuwa Gari lililobeba
Shehena ya Mabomba ya Kusafirishia gesi kutoka Mjini Mtwara kuelekea Dar
limeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva Wa lori hilo Kujeruhiwa
Vibaya. Lori hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika
manispaa ya mikinda Mtwara Mjini Sababu ya kushambulia gari hilo ni
katika kile kinacho dhihirisha kua wana Mtwara bado hawajakubaliana na
hoja ya Serikali ya kutaka Kusafirisha Gesi hiyo kwaajili ya Manufaa ya
Nchi.
Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi Mtwara, Ikiwani wiki moja tu imepita tokeaa watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka Dar.
Soma zaidi: http://mwanahabariuswazi.blogspot.com/2013/07/mtwara-wananchi-wacharuka-washambulia.html#ixzz2ZURRKEOt
No comments:
Post a Comment