Monday, 22 July 2013

MMILIKI WA FACEBOOK ALIWAHI KUHISI 50 CENT AMEFANYA KAZI KWAKE


 
 

 
50 Cents hajawahi kumaliza high school, lakini alishawahi kuaminiwa kuwa "mkuu wa maendeleo ya biashara  na mauzo" kupitia facebook 2005.
 

 
Wakati nafasi ya  mwanzilishi mwenza wa Facebook, Saverin Eduardo (mkuu wa maendeleo ya biashara  na mauzo) kuchukuliwa na
Kevin Colleran, Zuckerberg alimchanganya kijana huyo na mega superstar 50 Cent kutokana na picha ya profile yake inayomuonyesha akiwa na 5o Cent.
 

 

Hivi ndivyo jinsi ilivyokuwa siku ya kwanza walipokutana Zuckerberg na Colleran uso kwa uso..
 

 
Zuckerberg alipanga kukutana na Colleran mbele ya Virgin  Megastore iliyopo New York Union Square, Colleran alifika akiwa amechelewa na hivyo kuelekea moja kwa  moja alipo Zuckerberg huku akipokea simu kutoka kwa huyo huyo Zukerberg akimuuliza "Uko wapi", Colleran akamjibu nimpo mbele yako. Zuck alimuangalia kwa mshangao sana, alidhani muuza matangazo ya facebook ni yule jamaa aliekuwa akionekana  mweusi na tafu sana kwenye profile picture (50 Cents)
 

 
Rais wa Facebook na mwanzilishi wa Napster, Sean Parker alimwambia Colleran kuwa mkutano na Zuckerberg ulikuwa wired sana sababu "sisi tulidhani ungekuwa African-American."
 

 
Wakati wa mkutano wao, 50 Cent alikuwa tayari kashauzwa rekodi zaidi ya milioni 8 na album yake ya kwanza Get Rich Or Die Trying, na moja ya single zilizofanikiwa sana kwenye radio kwa muda wote  "In Da Club" na alikuwa kashasainiwa Dr Dre na Eminem.

No comments:

Post a Comment