Friday, 5 July 2013

WANAO TUMIA MITANDAO YA KIJAMIII VIBAYA KUKIONA CHA MOTO

MITANDAO ya kijamii imekuwa ni njia nyepesi ya kuwasiliana na kujifunza mambo mbalimbali ya kimaendeleo yanayofanyika ndani na nje ya nchi.

Mitandao hii imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuteka akili za watu wa rika zote wadogo kwa wakubwa, kila mtu akitumia mitandao kulingana na dhumuni, mahitaji na akili zake zinavyomtuma.

Ilivyo sasa ni kwamba mitandao hii imekuwa huru kwa kiasi kikubwa hali inayochochea mmomonyoka wa maadili kwa jamii hasa watoto wadogo wanaoingia kwenye mitanadao hiyo wakiwa hawana usimamizi wa kuwaongoza kuangalia kipi na wasiangalie lipi.

Sipingani na matumizi ya mitandao hiyo kwani ndiyo maendeleo tunayoyatafuta ila umefika wakati wa kuangalia na kuzingatia mambo yanayopaswa kufanyika kwa lengo la kuepusha usumbufu ama kutokuelewana kwa jamii ya watanzania.

Wapo wanao tumia mitandao hii kwa kujifunza na kujipatia maarifa, pia wapo baadhi ya watumiaji na tovuti zenye lengo la kupotosha jamii na kusababisha lawama na usumbufu kwa watu binafsi ama taasisi za umma.

Naeleza wazi kuwa hizi jitihada zetu za kugeuza dunia kuwa kijiji kwa Tanzania zimeanza kuonesha madhara ikiwemo wizi kwa njia ya mitandao, mmomonyoko wa maadili kwa jamii pia kudhalilishana jambo ambalo ni kinyume na utamaduni wetu ma lengo la kuwepo mitandao hiyo.

Mambo haya hayajaishia hapo kwani kila kukicha mambo yanaendelea kuongezeka kwenye mitandao, imefikia hatua ya kuwadanganya wananchi kuchukua machapisho kwenye tovuti nyingine na kuondoa au kuongeza baadhi ya maneno hali inayosababisha lawama baina ya pande mbili.

Ukweli wa mambo ni kuwa hivi karibuni Watanzania wametakiwa kujihadhahari na mitandao ya kijamii inayo andaa matangazo yanayohusiana na mchakato wa ajira katika utumishi wa umma kwani matangazo hayo si ya kweli.

Pamoja na Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tcra) kutanga kuwachukulia hatua za kisheria wamiliki wa mitandao wanaotoa habari za kughushi bado wamiliki hao wamekuwa na uthubutu wa kuchukua matangazo katika tovuti za Serikali na kuyahariri kisha kuyabandika kwenye kurasa zao bila woga.

Watu wanafanya hilo kwa makusudi lengo ni kupotosha umma huku wakijua wazi kuwa taarifa hizo wanazochapisha au kuziandika katika mitandao hiyo ya kijamii si sahihi na hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira.

Wanao tumia mitandao kupotosha waadhibiwe
Tangu July 4, 2013, na | Imesomwa mara 4 | Haina maoni
Prof-Makame-Mbarawa[1] 

Na Joyce Ngowi

Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Ajira, Xavier Daudi ndiye aliyesikika akilalamika kuhusu mitandao hiyo na kuitaja baadhi ikiwemo ule wa www.eastafricajobscareer.com ambao umetoa matangazo yanayoonesha mwisho wa kupokea maombi ni Julai 14 na Ogasti 10 mwaka huu.

Hadi sasa ni alimia 10 tu ya Watanzania ndio tunaotumia mitandao hiyo tupo wachache lakini tunaudanganyifu mwingi hivi tukifika asilimia 44 kama wenzetu wa Kenya tutakuwa upande gani? Pia tunapaswa kujiuliza na kutafuta majibu ya msingi kwa nini tunadanganya.

Tabia hii iachwe mara moja inaweza kuleta mafarakano katika jamii kwani dunia ya sasa kazi imekuwa ni bidhaa adimu kwa dunia nzima hivyo mtu anaposikia nafasi za kazi hasa katika sekta za umma akili na mawazo ya mhusika yanahamia juu ya mchakato wa upatikanaji wa ajira yenyewe, hivyo mtu anatumia muda mwingi kuhangaikia jambo lisilo la kweli. Hali hiyo haipendezi.

Pamoja na kuwataka wananchi wote kufahamu kuwa Sekretarieti hiyo ndiyo chombo pekee kilichoundwa kwa mujibu wa sheria kushughulikia mchakato wa masuala ya ajira katika utumishi wa umma itakuwa ni kazi nyingine hasa wasiofuatilia mambo na kujiridhisha ikiwa tangazo ni la kweli au si halali.

Ikiwa watu hawa wanakuwa na jeuri hata ya kuingilia shughuli za Serikali itakuwaje kwa wananchi na wale wasio na ufahamu wa mitandao wala njia za kujilinda.

Nionavyo ni kwamba usumbufu unaotoakana na matangazo ni kuwasababishia wananchi kero zisizo na msingi ambao wengi wao wanatafsiri kuwa Tume ya Ajira inatangaza nafasi za kazi na nafasi hizo zilisha kuwa na watu hivyo fursa hiyo imetumika kuhalalisha waliopewa nafasi hiyo.

Jambo hili linaweza kuleta msigano pande zote kwani kila mmoja atajiona yupo sahihi kwa nafasi yake hivyo wananchi wataiona Tume hiyo haiwatendei haki au kuelewa kuwa nafasi hizo zinapatikana kwa njia zisizo halali ilhali usaili unafanyika kwa kuzingatia vigezo vya muombaji na mahitaji ya nafasi zilizopo.

Wamiliki wa mitandao mnawajibu wa kusimamia mitandao yenu ili kuhakikisha wananchi hawapati usumbufu kupitia kwenye tovuti zenu.

No comments:

Post a Comment