Mtu wangu wa nguvu nakupa breaking news ambayo ndiyo kwanza imevuja huko Marekani inayomuhusu mwanadada Rihanna na rapper Drake. Kama ulikuwa hujui kuhusu Rihanna ni kwamba ameachana na Chris Brown ambaye ni hasimu mkubwa wa Drake hadi walifikia hatua ya kupigana kwenye night club. Habari za uhakika kutoka kwenye mmoja ya crew member wa Rihaana ambaye anasafiri naye kilaanapoenda, ameuambia mtandao maarufu wa udaku nchini marekani kwamba Drake na Rihanna wamerudiana. Snitch huyo amesema kwamba Drake amekuwa anapanda ndege na kwenda kwenye nchi ambayo Rihanna yupo mara kadhaa na ku-spend naye muda mrefu sana. Jamaa anaendelea kutoa info kwamba Rihanna akiwa na Drake anakuwa ni mtu mwenye furaha sana na kuna kila dalili za hawa wawili kwenye mapenzi tena. Jinsi ilivyokwa RIhanna huwaga hawezi kuficha kitu, so inategemewa kwamba hivi karibuni Rihanna ataweka wazi mahusiano yao hawa wawili.
No comments:
Post a Comment