Tuesday, 2 July 2013

MAHAKAMA YAWATIA MBARONI WAPENZI WAWILI WALIOAMUA KUTALII WAKIWA UCHI



Njemba moja, Stephen Gough aliyewahi kuwa mwanajeshi amekamatwa na polisi katika Jiji la Portsmouth, Uingereza baada  ya kukutwa na mpenzi wake wakidunda kutalii mitaani wakiwa uchi wa nyama.
Mwanamke Melodine Roberts aliyefuatana naye aliachiwa na polisi kwa kuwa mara baada ya kuonywa kuacha tabia hiyo, aliacha lakini mpenzi wake huyo aligoma na hii ni mara ya 14 akifanya hivyo licha ya kufungwa jela huko nyuma.   Baada ya kugoma polisi walimfunga pingu na wakampeleka mahakamani moja kwa moja  ambapo Mwendesha Mashitaka, Simon Jones alisema Gough alikuwa amekiuka sheria na aliwahi kufungwa miaka sita na moja ya makosa yaliyosababisha  afungwe ni kutemba uchi wa mnyama hadharani.
 
Baada ya maelezo hayo, jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Sarah Munro alisema kuwa kwenda jela kwa mtu huyo ndiyo ilikuwa njia pekee kwake kwa kuwa hilo ni kosa kubwa katika jamii ya Waingereza na ni ukiukwaji wa taratibu za umma wa sehemu hiyo.
 
Gough alikiri kosa hilo na hakujitetea na jaji akamfunga miezi kumi na moja jela.

No comments:

Post a Comment