Wednesday 31 July 2013

KODI YA SIMU KURUDI BUNGENI AGOSTI MWAKA HUU KWA AJILI YA KUJADILIWA UPYA


SAKATA la kodi ya simu ya Sh 1,000 kwa kila laini ya simu kwa mwezi, inayolipwa na watumiaji wa simu, litamalizwa bungeni kisheria. 


Waziri wa Fedha, William Mgimwa, amesema wameanza kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuitaka Wizara ya Fedha kukutana na wadau wengine, kuangalia namna ya kupata vyanzo vingine vya mapato mbadala wa kodi hiyo.


Alisema hayo alipozungumza jana na Habari leo, baada ya kusaini mkataba wa msaada wa zaidi ya Sh bilioni 344, kutoka Benki ya Dunia, ili isaidie masuala mbalimbali katika sekta ya usafirishaji. 
 
Mgimwa alisema katika suala hilo, masuala ya kisheria yatafikishwa bungeni mwezi ujao, ili kumaliza utata wa kodi hiyo.



Alisema uamuzi wa kushughulikia suala hilo, ulifikiwa kutokana na agizo la Rais Kikwete la hivi karibuni, kutaka wizara hiyo na ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kukaa na kampuni za simu kumaliza utata uliojitokeza kuhusu kodi hiyo.



Awali Umoja wa Wamiliki wa Kampuni za Simu (MOAT), ulitoa maoni kutaka kufutwa kwa kodi hiyo, kutokana na kulalamikiwa na wadau wa sekta ya mawasiliano.



Mbali na Moat, pia baadhi ya viongozi wa Serikali, wabunge na wananchi, walipinga kodi hiyo kwa walichokieleza kuwa itaongeza mzigo wa ugumu wa maisha kwa mtumiaji, hususan wa kipato cha chini.


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, alipozungumza na gazeti hili jana, alisema mara baada ya Rais kutoa agizo, wizara husika zilikutana kufanyia kazi agizo hilo.


"Rais akishaagiza kinachofuata ni utekelezaji na sisi kesho yake tulianza vikao na ninachoweza kukwambia tuko pazuri na tukikamilisha majadiliano yetu, tutatoa taarifa," alisema Makamba.



Alisema lengo ni kuangalia kama Serikali inaweza kupata Sh bilioni 178 kutoka vyanzo vingine, iwapo itaamua kufuta kodi inayotokana na tozo ya Sh 1,000 kutoka kwenye laini za simu.



Hivi karibuni, Rais Kikwete aliagiza Wizara za Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano na kampuni za simu za mikononi nchini, kukutana kutafuta jinsi ya kumaliza mvutano wa kodi hiyo.



Alitoa maelekezo hayo baada ya kukutana na viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na wawakilishi wa kampuni za simu za TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel. 


Rais alisema lengo kuu la mkutano huo, liwe kupendekeza jinsi ya kuziba pengo la Sh bilioni 178 ambazo zitapotea katika bajeti, iwapo kodi hiyo itafutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/14.



Aliwaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa hawezi kuifuta moja kwa moja kodi hiyo, bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo litakalotokeza, huku tayari Bunge limezipangia matumizi.



“Nakuombeni kaeni pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani tutajaza pengo hili la Sh bilioni 178, endapo tutakubaliana kuwa kodi hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi yenyewe ni ngumu,” alisema Rais Kikwete.
Habari Leo

MONALISA AGOMA KUOLEWA TENA BAADA YA NDOA 5 KUVUNJIKA


Msanii mkongwe  kwenye  soko  la  filamu  Tanzania,Yvonne Cherry "Monalisa"  amesema  hatarajii  kuolewa  tena  baada  ya  kuvunjika  kwa  ndoa  zake  kadhaa  ikiwemo  ile  ya  producer  Tyson....
Akisimulia  mikasa  ya  maisha  yake  mbele  ya   mwandishi  wetu,Monalisa  aliema  kuna  siku  walipokuwa  kwenye  kikao  cha  sendoff  ya  mama  yake, alitania  na  kusema  ataolewa  disemba  lakini  hakuwa  serious....
"Sina  mpango  wa  kuolewa  kabisa,kwanza  sina  mchumba, ntaolewaje?
"Siku  ile  nilikuwa  natania  tu kwa  sababu  sipo  tayari  kuolewa  na  kuachika  tena"..Alisema  Monalisa

WAASI WA M23 WAPEWA MASAA 48 YA KUSALIMISHA SILAHA ZAO.....VINGINEVYO NI BALAA TUPU

 
Wanajeshi wa Brigedi Maalum wakiwa katika mazoezi makali yaliyofanyika hivi karibuni huko Goma Mashariki ya Demokrasia ya Kongo..
 Mmoja wa walinda amani kupitia Brigedi Maalum inayoundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika ya Kusini na Malawi akiwa katika moja ya mazoezi yaliyofanyika hivi karibu huko Goma.
 Kamanda Mkuu wa Misheni ya Kulinda Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ( MONUSCO ) Luteni Jenerali Carlos Albeto dos Santos Cruz ametakanza jana jumanne akiwa Goma kwamba MONUSCO itaanza rasmi kuitumia Brigedi Maalum na ametoa saa 48 kuanzia saa kumi jioni kwa saa za Goma jana siku ya Jumanne waasi wote kusalimisha silaha zao, na kwamba ifikapo saa kumi jioni kwa saa za Goma siku ya Alhamisi Agosti Mosi wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio la usalama kwa wananchi na MONUSCO italazimika kuwapokonya ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kwa mujibu wa Mamlaka iliyopewa na Sheria zinazowaruhusu kufanya hivyo.
----------------

Misheni ya Kutuliza   Amani katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  ( MONUSCO) imetangaza  kwamba kwa mara ya kwanza itaanza kuitumia Brigedi Maalum ( Force Intervention  Brigade)  katika kudhibiti  eneo  maalum  la usalama  ( security zone ) kuzunguka  mji wa Goma ulioko   Mashariki ya  Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo na imewapa  saa 48 waasi kusalimisha silaha zao.

Taarifa iliyotolewa na  MONUSCO na kusambazwa na   Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa  jana  jumanne,  inaeleza kwamba watu binafsi katika eneo la   Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na  Sake  na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama watapewa saa 48 kuanzia saa kumi jana kwa saa za Goma ( Jumanne ) kuzisalimisha silaha zao katika  Misheni hiyo na  kujiunga na mchakato wa DDR/RR unaoratibu upokonyaji, usambaratishaji,  urejeshwaji makwao, kuwaunganisha  na jamii na kuwapatia makazi.  

Baada ya  saa  kumi jioni ya  Alhamisi, Agosti Mosi. Taarifa hiyo inasema. Wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama  tishio kwa usalama wa  wananchi na MONUSCO itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja  na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika Mamlaka na sheria za  ushiriki  za  MONOSCO. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kando kando ya barabara  ambayo inawaunganisha na   kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo ni  makazi ya  muda ya watu  karibu 70, 000 ambao wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.

Kwa mujibu wa MONUSCO, tangu kati kati ya mwezi Mei eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la M23 dhidi ya  majeshi ya Serikali  ya  FARDC ikiwa ni  jaribio la   wazi la kutaka  kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.

“ Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia  kiholela silaha zao  za  moto zikiwamo silaha nzito  ambazo zimesababisha  wananchi kujeruhiwa” .
Taarifa hiyo imeongeza kwamba    kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo  limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.
Aidha  taarifa hiyo inabainisha kwamba  eneo hilo maalum la usalama ( security zone)  litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja  mbali na eneo la  nje ya Goma na pengine  eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa sehemu  nyingine  kutakako hitajika.
 Tamko hilo  la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha zao  linafuatia kuwasili  katika eneo la Goma kwa  Kamanda Mkuu wa  MONUSCO, Luteni    Jenerali  Carlos Alberto dos Santos Cruz, ambaye alitangaza kwamba  Misheni ya MONUSCO itaunga mkono jeshi la Serikali  ( FARDC)  katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma  eneo la  Goma na vitongoji vyake.
 
Taarifa hiyo inamkariri Kamanda  Mkuu wa MONUSCO akiyapongeza  majeshi ya serikali  kwa  kazi nzuri iliyofanya wiki  iliyopita ya kuwadhibiti M23. Ingawa  anasema eneo la Goma na Sake   bado limo katika mazingira magumu sana na kwamba ni wajibu wa wahusika wote kuhakikisha wahalifu wote hawaendelei kuhatarisha  raia wa eneo hilo.
Kwa mwaka uliopitia , kundi la M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yamekuwa yakipambana mara kwa mara na majeshi ya serikali katika  Mashariki ya Kongo, huku  makundi hayo yenye silaha  mwezi Novemba mwaka jana yakiikalia Goma  kwa muda.
Aidha mapingano ya hivi karibuni  ambayo safari hii yalihusisha pia kundi jingine la wanagambo wenye silaha  lenye asili yake nchini Uganda, yamesababisha zaidi ya wananchi 100,000  kuyakimbia makazi yao na hivyo kuongeza mgogoro  wa kibinadamu katika eneo hilo linalohusisha watu wengine 2.6 milioni ambao wameyakimbia makazi yao huku wengine 6.4 milioni wakihitaji  chakula na  huduma za dharura.
Wakati huo huo,   Kaimu Mkuu wa  MONUSCO  Bw. Moustapha Soumare  katika taarifa  yake ametoa wito kwa pande zote kutafuta suluhu ya kisiasa  kwa   matatizo ya  DRC kupitia Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama  na  ushirikiano wa maendeleo katika DRC na  eneo la Maziwa  Makuu uliopitisha mwezi wa Februari na viongozi 11 wa Afrika na  Taasisi nne za  Kikanda na Kimataifa.

Aidha akasema  katika  kipindi hiki ambacho suluhu la kisiasa linatafutwa MONUSCO itatumia nguvu iliyonayo kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zitokanazo na  makundi ya waasi.

ROSE NDAUKA ANASWA AKIPAPASWA NDANI YA GARI KABLA YA KUPELEKWA HOTELINI

 
Rose Ndauka  au  Aisha  anaweza  kuwa  ameitia  najisi  funga  yake  baada  ya  kunaswa akiingia  hotel  moja   iliyoko  kinondoni  jijini  Dar  kwa  kile  kilichoelezwa  ni  kwenda  kuivunja  amri  ya  sita  na  mwanamziki wa  bongo  fleva  Nassoro  Ayoub  "Nasry"   au  Tajiri Boy
 
Rose ambaye alisilimu mwaka jana  na  kupewa  jina  la  Aisha  baada  ya  kuchumbiwa  na mwanamziki  mwasisi  wa  kundi  wa  TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na  kamera  za wakazi wa jirani na  hoteli  hiyo  mwishoni  mwa  wiki  iliyopita.....

Shuhuda  wa  tukio  hilo  amedai  kwamba  majira  ya  mchana  kweupe  gari  aina  ya  Toyota Mark  X lenye  rangi  nyeusi  liliwasili  kwenye  viunga  vya  hoteli  hiyo  na  kusimama  kwa  takribani  dakika  10  kisha  likaondoka  na  kwenda  kupaki  sehemu  nyingine  ambapo  ni  umbali  mfupi  toka  hotelini  hapo...
  Kitendo  hicho  kiliibua  mashaka  miongoni  mwa  watu  hasa  kutokana  na  vioo  vya  gari  hilo  kuwa  tinted  hivyo  kutowaonesha  waliokuwemo  ndani...

"Walipoondoka  na  kupaki  palipojificha  tuliamua  kuwasogelea  ili  tujue  ni  akina  nani

"Baada  ya  muda, kioo  cha  dereva  kilishushwa kidogo, tukamuona  dogo  anayefanana  na Diamond  akiwa  anampapasa  demu  aliyekuwa  pembeni  yake...

"Tulipoona  hivyo, tulidhana  mnyamwezi  ameamua  kumaliza  mambo  yake  ndani  ya  gari, hivyo  tukaziweka  simu  zetu  standby  kwa  ajili  ya  kushuhudia" alisema shuhuda  huyo

Baada  ya  muda, mlango  wa  kulia  ulifunguliwa  kisha  wakamuona  dogo  aliyetambuliwa  kwa  jina  la  Nasry

"Kumbe  hakuwa  Diamond,alikuwa  ni  dogo  Nasry.Tulipotupa  jicho  ndani, tulihamaki  kumuona  Rose  Ndauka  akibadili  nguo  na  kujitanda  baibui.

"Nadhani  alifanya  hivyo  ili  watu  wasimjue  pindi  atakaposhuka  kwenye  gari  maana  aliposhuka  tu, waliongozana  na  dogo  Nasry  kwa  mwendo  wa  kasi  hadi  ndani...

"Toka  walipoingia  ndani  hadi  walipotoka  iliwachukua  kama  masaa  matatu  hivi.Wakati  wa  kutoka, Nasry  alilifuata  gari  hadi  mlangoni  na  kisha  Rose  akaingia  na  kutokomea"...Kilimalizia  kusimulia  chanzo  hicho

Tuesday 30 July 2013

CHADEMA HAINA UBAVU WA KUMKATAA TENDWA


OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina ubavu wa kumkataa au kutomtambua John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasai, Rajab Baraka alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliyedai chama hicho hakimtambui John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa.

Katika madai yake Dk. Slaa alidai Tendwa anakipendelea CCM katika kutoa haki ya demokrasia na hatendi haki kama mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini.

Dk. Slaa alisema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kusisitiza hata katika barua zao za mawasiliano kwenda kwa ofisi ya msajili chama hicho hakitumii jina la John Tendwa.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Chadema kinaitambua ofisi ya Msajili wa Vyama tu lakini hakimtambui Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

“Hatumpelekei hata barua huyu hatunzi sheria siyo mtu wa kulea vyama ni mlezi wa chama kimoja, hayuko serious na hatushirikiani naye mpaka aondoke madarakani.

“Tukiandika barua hatuweki jina lake lakini tunaitambua ofisi yake, hata yeye mwenyewe analijua hilo na akijibu barua zetu haweki jina lake,” alidai Dk. Slaa.

Akijibu hoja hizo, Naibu Msajili alisema Chadema hawana ubavu wa kutomtambua Tendwa kwa sababu amewekwa kisheria na ofisi yake ipo kisheria.

Alisisitiza Tendwa ataendelea kuwa mlezi wa vyama vyote na siyo chama kimoja kama inavyodaiwa na kuvitaka vyama vyote kuheshimu sheria iliyomuweka madarakani msajili huyo.

Mtanzania.

MBUNGE WA CCM ANAYEDAIWA KUFADHILI MADAWA YA KULEVYA AJISALIMISHA POLISI


Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.

Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike  na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan kwa njia ya simu


"Mimi sipo juu ya sheria ,  itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza:

 "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao," alinukuliwa Mbunge huyo.

WAPIGWE TU" YA MIZENGO PINDA ITAMFIKISHA KORTINI



KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake.
Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka.
Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea uvunjifu wa sheria.
Akitangaza kusudio la kituo hicho kufungua kesi dhidi ya Pinda, Mkurugenzi wa maboresho na utetezi, Harold Sungusia, alisema hadi jana walikuwa tayari wameandaa kusudio la shtaka lao.
Alisema kuwa kisheria kilichowafanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na waziri mkuu huyo kukiuka Katiba ya nchi inayozungumzia usawa mbele ya sheria.
“Kitendo alichofanya waziri mkuu cha kuwaruhusu polisi kupiga wananchi hakikubaliki hata kidogo na walitegemea kwamba angeomba radhi kutokana na kauli yake hiyo tangu alivyoshinikizwa kufanya hivyo na makundi mbalimbali.
“Badala yake ameendelea kuwa kimya licha ya mkubwa wake, Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni kukiri kwamba mtendaji wake huyo aliteleza,” alisema.
Sungusia aliongeza kuwa Alhamisi wiki hii wataweka bayana kwa waandishi wa habari ni wapi kesi hiyo itafunguliwa.
Pinda alitoa kauli hiyo tata ambayo imehojiwa na wengi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) aliyehoji kama serikali iko tayari kutoa tamko kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha, Mtwara na maeneo mengine pamoja na hatua ya vyombo vya dola kutumia nguvu.
Katika majibu yake Pinda alisema kuwa suala la amani linawagusa wote, kwamba jukumu ni kwa viongozi wa kisiasa. Alifafanua kuwa kama viongozi wa kisiasa hawatafika mahali wakakubaliana bila kujali vyama vyao nchi itafika pabaya.
Pinda alifafanua kuwa kwa upande wa serikali lazima wahakikishe kwamba wale wote wanaojaribu kuvunja amani kwa namna yoyote ile kazi waliyonayo ni kupambana kweli kweli kwa njia zozote zinazostahili.

“Mimi naomba sana Watanzania, maana kila juhudi zinazoonekana zinaelekea huko, tunapata watu wengine wanajitokeza kuwa mara unajua…unajua. Acheni serikali itimize wajibu wake, kwa sababu jambo hili ni la msingi na wote tulilinde kwa nguvu zetu zote.

“Mheshimiwa Mangungu umeanza vizuri lakini hapa unasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo unaambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi, utapigwa tu,” alisema.
Waziri mkuu aliongeza kuwa hakuna namna nyingine, maana lazima watu wakubaliane na serikali kwamba nchi hii wanaiendesha kwa misingi ya kisheria.

“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ni jeuri zaidi, watakupiga tu, na mimi nasema wapigwe tu, maana hakuna namna nyingine, tumechoka,” alisema
tanzania daima

WAKUTWA NA MAUTI WAKIFANYA MAPENZI.

Kwa Mujibu wa Ripoti iliyotolewa na wakazi wa eneo husika, inasemekana kwamba Bw. Mathias Nwoko,45, na Binamu yake Angela Ihuoma walifikwa na Umauti wakati wakiwa katika tendo la ndoa.
Wawili hao ambao asubuhi kabla ya kufariki walionekana pamoja wakicheza kwa furaha katika sherehe za kumkaribisha Padri Mpya katika Jimbo lao, Mathias ambaye ameelezwa alikuwa ndani ya ndoa kwa kipindi cha miaka 13 bila ya kupata mtoto alirudi na binamu yake usiku wakitokea kusikojulikana na kumkuta mkewe akiwa anaangalia T.V nyumbani kwake.
Mathias alimwambia mkewe atangulie kulala kwasababu yeye anachukua tochi amsindikize binamu yake huyo kwao. Mama mzazi wa Angela alipoona usiku unazidi na mwanawe hajarudi alimtafuta kupitia simu yake ya mkononi ambayo alipokelewa na Mathias akimwambia wapo pamoja.
Mpaka asubuhi, Si Mathias wala Angela Aliyerudi kwao na ndipo familia zote mbili zilipoingiwa na wasiwasi, Mke wa Mathias alienda katika nyumba yao ya pembeni asubuhi hiyo na ndipo alipowakuta wawili hao, mwanamke akiwa juu ya mwanaume.
Aliganda kwa muda asiamini anachokiona,hasa kuona wawili hao hawashtuki japo kawaona na ndipo alipogundua ya kwamba wamefariki Dunia. Ilibidi kutoa taarifa kwa familia ya Angela ambapo alikuja mama yake mzazi ambaye alipigwa na butwaa kutokana na picha iliyokuwa mbele yake.
Miili yao ilitenganiswa na kupelekwa hospitali huko Ogbor Nguru, jimbo la Aboh Mbaise

Monday 29 July 2013

HII NDIO PETE YA UCHUMBA ALIYOONEKANA NAYO RAPA NICK MINAJ BAADA YA DJ KHALID KUMUOMBA KUMUOA RICK ROSS NAYE ALONGA


1Baada ya Dj Khaled kutokea MTV akitangaza mapenzi yake ya dhati kuhusu nia ya kumuoa Nicki Minaj, mrembo huyu wa Young Money ameonekana Crustacean Restaurant Los Angeles Marekani akiwa na pete ya uchumba kwenye mkono wake wa kushoto wakati alipotoka kula chakula cha jioni na baadhi ya marafiki zake waliosoma pamoja High school.
Unadhani hiyo pete kavishwa na Khaled????!!! Biiig No…. kwa mujibu wa Necole hii ni pete ambayo inaaminika alivishwa na boyfriend wake wa longtime kitambo anaitwa Safaree ambae nae amekua akionekana kavaa pete kama hiyo ya gold ambayo imesababisha watu waamini pia uwezekano wa ndoa ya siri ya wawili hawa.
2
3
Dj Khaled na huu mpango wake wa kutangaza nia ya kumchumbia Nicki Minaj aliiambia Power 106 kwamba anampenda sana Nicki Minaj kama ambavyo wanaume wengi wamekua wakivutiwa kumuoa pia, lakini akasisitiza kama Nicki atakataa kuchumbiwa na yeye… hakutakua na ubaya, bado ni marafiki…
Namkariri akisema ‘Nicki anaweza kutokua tayari kwa ndoa ila nitamwambia ninachofeel, hata akisema ndio kwangu au akiniahidi mwakani nitasubiri tu, sitokata tamaa… nataka watoto’
Dj Khaled
Rapper Rick Ross ambae ni rafiki wa wote Nicki Minaj na Dj Khaled ametoa baraka zake kama ni kweli hiyo ndoa ipo na miongoni mwa aliyoyasema ni uwezekano wa kuwapa gari kama zawadi ya harusi yao, mchek zaidi kwenye video hapa chini ambapo mpaka anahojiwa hapa alikua hajaiona video ya Dj Khaled akiomba uchumba kwa Nicki huku akiwa na pete mkononi.

SIJAWAHI PIGA PICHA ZA UCHI...NIMEMFAHAMU SINTAH KUPITIA SKENDO YA KUGAWA PENZI KWA NATURE"...RAYUU AFUNGUKA TENA


Jana, Bongomovies.com imefanya interview kwa njia ya simu na mwanadada msanii Rayuu alaice Bungenzi kuhusiana na mambo mablimbali yanayoandikwa kwenye mitandao na tovuti mbalimbali nchini. 


Katika interview hiyo waliweza kupata mambo manne  kama  ifuatavyo:

 

1. Hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza ili kupata umaarufu



Akiongea kwa msisitizo Rayuu amesema kuwa hajawai kupiga picha za utupu na kuzisambaza kwenye mtandao kwa ajili ya kupata umaarufu.



“Sijawai kusambaza picha za utupu ili nipate umaarufu, hizo picha kweli ni zangu na ukizitazama vizuri sio picha za utupu kama watu wanavyosema(?????), ni picha nilizopiga kwenye simu yangu kujiangalia tattoo yangu niliyochora kiunoni lakini kuna marafiki zangu waliochukua simu yangu na sijui ni nani ndio zilisambaa kutokea hapo na kila mtu kuandika stori anayoijua yeye” Alisema.




2. Hafahamiani na wala hajawai kuonana na sintah kwa zaidi ya miaka mingi sana



Rayuu amesema kuwa hajawai kuonana na sintah, wala hafahamiani naye personally na huwa anashangaa sana kwanini mwanadada huyu anamchafua kwenye blog yake.




“Kiukweli mi sifahamiani na Sintah, na wala hatujawahi kuonana kwa kipindi kirefu sana, sasa huwa nashangaa kwanini ananichafua na kunitukana kwenye blog yake. Kuna kipindi nilichoka nikaanza kumjibu lakini baadaye nikaona ni utoto bora ninyamaze kwanza nione kama ataacha lakini nashangaa hakui.



Huyu dada mi huwa simuelewi kwakweli,anagombana na kila mtu, nahisi anaweza kugombana hata na panya. Kwanza ni mtu mzima sana kwangu. 



Nakumbuka mi nimemfahamu yeye wakati teyari kashakuwa maarufu na skendo za uroda kwa Juma nature na mimi nilikuwa bado mdogo sana. Sa sijui kwanini hakui. Kila siku anatukanwa kwenye blog yake lakini wala hajali.”…Alisema Rayuu



3. Marehemu Mzee Kipara ndiye haswa aliyemuingiza kwenye sanaa


Watu wengi hawajui kuwa marehemu mzee kipara ndiye aliyemuingiza Rayuu kwenye sanaa. Rayuu alisema kuwa anakumbuka siku moja kundi la kaole walienda kurekodi igizo  lao mitaa ya nyumbani kwa kina Rayuu na alipowaona alimfuata mzee kipara na kumueleza nia yake na ndipo alipompeleka na kumtambulisha kwenye kundi la kaole na kuanza kupata nafasi ya kuigiza na kufanya mazoezi kundini hapo.



4. Sio mtu wa kutoka sana na akila "bata" anaumwa sana kesho yake


Rayuu amesema yeye sio mtu wa kutoka na kupenda kwenda club kama wengi wanavyodhani bali hupenda sana kushinda ndani kwani akifanya hivyo kesho yake lazima aumwe siku nzima


-bongomovies.com


JACK WOLPER AMJIBU MBAYA WAKE ALIYETANGAZA KUWA YEYE NI KAHABA


 
Msanii  nyota  wa  filamu  bongo, Jacqueline Wolper   amewataka  wasanii wa  bongo  movie  kuacha  tabia  ya  kupigana  majungu  ya  kinafiki  ambayo  huchangia  kujenga  bifu  za  kijinga....


Akiongea  na  mpekuzi  wetu, wolper  alidai  kuwa  kuna  mipaka  ya  watu  kuishi  lakini  kuna  baadhi  ya  wasanii  wanaamini  kwamba majungu  ndo  mshahara  wao  kiasi  kwamba  wasipomsengenya  mtu  basi  hawawezi  kuishi...


Wolper  anadai  kuwa   yeye  ni  miongoni  mwa  wasanii  wanaosemwa  sana  kwa  mabaya  hasa  kuhusu  maisha  yake  ya  kila  siku.Hali  hiyo  inatokana  na  umaarufu  alionao  ambao  huwafanya   wasanii  wenzake  wamchukie  hasa  wasanii  wa  kike...




  Hii  ni  kauli  ya  Wolper  alipoongea  na  mpekuzi:

"Wasanii  tungekuwa  na  ushirikiano  kama  nisha  tungefika  mbali  sana.


"Mimi  simuogopi  mtu  katika  maisha  yangu, lakini  ninachohitaji  katika  maisha  yangu  ni  Heshima.


"Ukiona  nimekukwaza, basi  njoo  nyumbani  au  nambie  nikufuate  ili  tuyamalize  kibinadamu  na  si  kudhalilishana  mitandaoni...


"Kuna  msanii  mmoja  wa  kike  amekuwa  akinichafua  sana  mitandaoni   kwa  kuniita  kahaba, najuza  na  matusi  mengine  kibao.


"Huyo  ni  mtu  anayetafuta  pakutokea, anatafuta  kujulikana  kupitia  Wolper  na  pengine  kafulia  na  sasa  anatafuta  mtaji.


"Tangu  anitukane  sikuona  haja  ya  kumjibu  kutokana  na  heshima    niliyo  nayo  katika  kazi  yangu  na  heshima  yangu  kwa  wazazi , ndugu  na  jamaa.


"Niliamua  kumwachia  mungu.Kama  ni  kahaba  au  najiuza, mungu  anajua.Alisema  Wolper 


MBUNGE IDD AZZAN 'NITAJIUZULU NAFASI ZANGU IKIBAINIKA NAUZA MADAWA YA KULEVYA"


MBUNGE wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya. Kauli hiyo imekuja siku
chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan.
Akizungumzia kuhusu sakata hilo jana, alisema hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla.
Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana jambo limejificha.
“Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwanini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo.


“Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.
“Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernad na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.


“Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu,” alisema Azzan.

Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.

“Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni,” alisema Azzan.

Alipoulizwa kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, alisema atakachokifanya anamuachia Mungu.

“Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua,” alisema Azzan.

Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa kupitia mitandao, ziliripoti kukamatwa kwa Watanzania wawili nchini China wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Dola milioni 3.34 za Marekani.

Wednesday 24 July 2013

KIWANDA CHA KUTENGENEZA SILAHA TANZANIA CHAGUNDULIKA


Kiwanda cha kienyeji cha kutengeneza vifaa na silaha mbalimbali,kimegundulika kuwepo jijini Dar es Salaam,ambapo wahusika wa kiwanda hicho wamekiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambayo yamesababisha mauaji mengi sehemu mbalimbali. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, kamishna msaidizi wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam DCP Ally Mlege,amesema katika hali ya kushangaza baada ya kukamatwa kwa baadhi ya watuhumiwa waliokuwa wakijihusisha na matukio ya ujambazi,hatimaye baada ya kubanwa na jeshi la polisi walikubali na kusema kiwanda hicho kilichopo maeneo ya Kawe Mzimuni kinatumika katika kutengeneza na kukarabati vifaa na silaha mbalimbali zinazotumika katika matukio ya uporaji na unyang'anyi ambavyo vilitumika na kusabisha mauaji mengi sehemu mbalimbali.
Aidha tapeli hatari bwana Mfaume Omary maarufu kwa jina la Mau(29)mkazi wa Magomeni Kagera,ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kutumia namba tofauti za mitandao ya simu na majina ya watu maarufu ikiwemo viongozi wa serikali na viongozi wa dini kwa lengo la kujipatia fedha kwa kuvaa uhusika wa mtu husika bila wanaombwa fedha hizo kugundua.
Jeshi la polisi limekanusha vikali kuhusu habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari kuwa mbunge wa jimbo la Ubungo Mh John Mnyika amekoswa na bomu na kumjeruhi moja ya wafuasi wake kuwa ni la huzushi,na ukweli ni kwamba bomu hilo lililipuka ndani ya gari la polisi Pt .1902 wakati askari dcp Julius alipokuwa ndani ya gari akisogeza box lenye mabomu ya machozi na kwa bahati mbaya bomu hilo lililipuka ndani ya gari hilo lakini halikuleta madhara kwa askari polisi yeyote wala raia waliokuwa katika eneo hilo

VAZI LA NUSU UCHI LAZUA MTAFARUKU KANISANI....PADRI AGEUKA MBOGO NA KUTIMUA WAPAMBE


KIVAZI cha ndugu wa maharusi, kimesababisha patashika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Peter, baada ya Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Padri Paulo Haule, kusitisha ibada mpaka mhusika atoke akavae vizuri.

“Ninatoa dakika 10 kwa aliyeingia na mavazi ambayo hayatakiwi kanisani humu kutoka mara moja akavae vizuri, la sivyo ndoa yao haitafungwa,” alisema Padri Haule wa Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.
Awali vurugu hizo zilizotokea Jumamosi iliyopita, zilianzia nje, wakati Katekista wa Parokia hiyo, Yohane Maboko, alipotangazia wanandoa na ndugu zao waliokuwa mabega wazi au kuvaa nguo fupi, kutafuta nguo za kujifunika au wasiingie kabisa kanisani.
Maharusi walikubali kutekeleza ombi hilo, wakavishwa vitambaa mabegani vya rangi tofauti na gauni jeupe la harusi, wakaruhusiwa kuingia kanisani, tayari kufunga pingu zao za maisha.


Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa maharusi hao ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipotaka kulazimisha kuingia na kivazi chake cha mabega wazi, alizuiwa na Katekista Maboko. Katekista huyo alimfuata mwanamke huyo ili kumrudisha akavae vizuri, lakini aliibua zogo na kulazimisha kuingia na vazi hilo.
Zogo hilo lilipoendelea, wanandugu waliingilia kati, wakitetea vazi hilo ambapo mmoja wa wanandugu, alimvua miwani Katekista Maboko na kuipiga chini ikavunjika huku yeye na wenzake wakimtolea maneno makali ya kumtaka asimzuie ndugu yao kuingia kanisani.
Wakati ndugu hao wakimdhibiti Katekista Maboko, mwanamke huyo alitumia mwanya huo na kupenya hadi ndani ya Kanisa, ambamo Padri Haule, alikuwa akijiandaa kuanza ibada.
Baada ya Padri Haule kupata taarifa, alitangaza kuwa ndoa ya maharusi wa msichana huyo, haitafungwa hadi awe ametoka.
Licha ya Paroko kutangaza hivyo, bado ukaidi uliendelea jambo lililomfanya Katekista Maboko kumfuata tena dada huyo na kumwamuru atoke nje, ambapo aliendelea kupinga na baadaye akatekeleza amri hiyo ya Paroko.
 Baada ya hapo shughuli za kufungisha ndoa ziliendelea kwa amani na utulivu hadi mwisho maharusi wakatoka kwenda kuendelea na mambo mengine.
Akizungumza na mwandishi wetu, Katekista Maboko alisema waumini hao walikiuka maadili ambayo Kanisa lina wajibu wa kulinda na kuyasimamia ili waumini wake wayafuate.


Alisema miwani yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya Sh 90,000 na baada ya ibada hiyo, aliyetenda kosa hilo alimwendea na kumwomba radhi na kulipa Sh 50,000 na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki wakati wowote.


Maboko alisema uvaaji wa mavazi yasiyotakiwa kanisani hapo, umekuwa ukipigiwa kelele mara kwa mara, na hata katika mafundisho ya ndoa huambiwa lakini ukaidi unaendelea.

“Maharusi wakati wa mafundisho ya ndoa tunawaambia kuhusu mavazi yao na hata ya ndugu zao watakaowasindikiza kanisani, kuwa wavae kistaarabu lakini hawasikii,” alisema Katekista Maboko.
Makanisa mengi siku hizi yamekuwa yakipiga marufuku uvaaji wa nguo fupi na zinazoacha mabega wazi kwa wasichana na wanawake, wakati wa ibada za kawaida na za ndoa.
Habarileo