Saturday 18 May 2013

MJENGO WA NISHA NOMA ZAIDI YA ULE WA WEMA

Shuka nayo apa.....   RISASI LATUA KIJITONYAMA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilisaga soli hadi maeneo hayo na kuanza kugonga geti moja baada ya lingine hadi lilipofanikiwa kuinasa nyumba hiyo huku Nisha akiwa ndani kapumzika.
Msichana aliyejitambulisha kuwa ni dada wa kazi au hausigeli kwa lugha laini ndiye aliyetoboa siri kuwa ni kweli staa huyo yupo ndani na amehamia mahali hapo muda si mrefu.
 
Ndani ya nyumba hiyo yenye vyumba vitano, sebule, jiko, choo na mabafu mawili, anayeishi Nisha na dada wake wa kazi, kuna samani nyingi za bei mbaya, mazagazaga kibao, mazulia na marumaru huku kila kona kukiwa na Tv ya flat screen hadi chooni (angalia picha Uk.1).

Nisha anayemiliki kampuni ya kuzalisha muvi za Kibongo ya Nisha’s Film Production alipotakiwa kueleza kama kanunua, kanunuliwa au kapangisha nyumba hiyo, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni juhudi zangu binafsi jamani, kujituma sana kwenye kazi yangu ya filamu. Kuhusu kununua au kupangisha naomba nikimaliza ‘process’ f’lanif’lani ndipo nitaweka wazi, kwa sasa bado ni mapema mno.”

No comments:

Post a Comment