Saturday 29 June 2013

WATU KUMI WAUAWA SOMALIA



Wakaazi wa mji wa Kusini wa Somalia Kismayo wanaendela kukikmbia makwao, kutokana na mapigano makali kati ya mababe wa kivita katika eneo hilo.

Takriban raia kumi wameuawa katika mapigano hayo yaliyotokea siku ya Ijumaa
Mji wa Kismayo ni mji muhimu wa kiuchumi Kusini mwa Somalia na vita hivyo vimechochewa na ushindani mkali wa kithibiti biashara katika mji huo wa bandari.
Ripoti zinasema wapiganaji wa kundi la Ras Kamboni wanaoongozwa na mbabe wa zamani wa kivita aliyejitangaza kuwa rais wa eneo hilo Ahmed Madobe walikabiliana vikali na wapiganaji wa waziri wa zamani wa ulinzi wa Somalia Bare Hirale, ambaye pia anaongoza kundi lingine la waasi katika eneo hilo.
Hali ya Utulivu imeanza kurejea tena mjini humo ambao ni ngome ya zamani ya kundi la kigaidi la Kiislamu la Al Shabaab ambalo lina uhusiano na kundi la Al-Qaeda.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay ametoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo mara moja, na kutoa wito kwa mababe hao wa kivita kusitisha uhasama kati yao ili kuepusha maafa zaidi ya raia wasiokuwa na hatia.
Wanajeshi wa Kenyan wanaohudumu nchini humo chini ya muungano wa Afrika wanamuunga mkono Bwana Madodbe, lakini serikali ya Somalia halimtambui kama rais na pia haijakubali uamuzi wake wa kutangaza kuwa eneo hilo limejitenga na Somalia.

OBAMA AKUTANA NA RAIS ZUMA


Rais wa Marekani Barack Obama, amesema uvumilivu na ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na upendo wa dhati wa rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni kwa namna gani alivyo na utu wa kibinadamu.
Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha ukweli na ukakamavu ambao una maana kubwa katika utu wa kibinadamu ambao uliondoa tabaka la ubaguzi, udini na utaifa.
Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria baada ya mazungumzo na rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
Ziara hiyo ya bwana Obama ina lengo la kuongeza mauhusiano ya kibiashara lakini imetekwa na hisia za ugonjwa wa bwana Mandela ambaye amelazwa hospitalini kwa muda wiki tatu sasa kutokana na maradhi ya mapafu yanayosumbua mfumo wake wa kupumulia.


Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela
Katika kikao hicho wawili hao walizungumza na vyombo vya habari kuhusu ushirikiano wa mataifa yao kibiashara mbali na kutafuta suluhu ya kudumu katika mataifa yaliokumbwa na ghasia mashariki ya kati.
Ikulu ya White House imesema kuwa Obama pia atakutana na familia ya Mandela anayeugua maambukizi ya mapafu ili kuifariji.
Awali Rais Obama, aliye ziarani barani afrika alitoa shukran za dhati kwa uongozi ulioonyeshwa na Mandela.
Wakati wa ziara hiyo Obama pia atakutana na wanafunzi huko Soweto kabla ya kuelekea katika jela la Robben Island ambayo Mandela alihudumia kifungo chake cha miaka 27 wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi.

DIVA WA CLOUDS FM AMVAA TENA HUDDAH....KISA NI PENZI LA PREZZO



Kama utakua ni muumini wa twitter lazima utakuwa unajua kinachoendelea kati ya mshiriki wa BBA kutoka Kenya (2013), Huddah na mtangazaji Diva Loveness love.
kiufupi ni bif kupitia twitter kisa kikiwa ni CMB Prezzo

Katika interview iliyofanywa  na Huddah, mrembo huyo wa Kenya  amesema hana uhusiano na Prezzo, ni rafiki yake tu, na hana beef yoyote na Diva na kwanza hamfaham.

"you know mimi hupenda kutoa maoni yangu, so saa ile mi natoa maoni yangu mtu ana-judge vingine, mi sina bif na Diva, na simjui, na kama uli-notice i only replied three times."

unajua mi niliandika "lol" after seeing her tweet calling Prezzo "baby", why? i just find it funny, so yeye ndio akawa anaandika all that" amesema Huddah

kwa inavyoonekana Diva alikua akisikiliza radio wakati interview ikiendelea, na haikumchukua dakika nyingi , akaibuka  katika  mtandao wa twitter:

OBAMA ATOA SABABU ZILIZOMFANYA ASIENDE KENYA KWA SASA... SABABU KUBWA NI KESI YA UHURU KENYATTA NA MAKAMU WAKE



US President Barack Obama said Saturday the “timing was not right” for him to travel to Kenya, his father’s homeland, during his current Africa tour, but he expected to go there many times in the future.

Obama said the new government of President Uhuru Kenyatta was still finding its feet after an election in March, and that Nairobi was “still working out issues with the international community”.

He was referring to a looming trial for Kenyatta and Vice President William Ruto at the International Criminal Court for their alleged roles in deadly violence that killed more than 1,000 people after 2007 polls.

“The timing was not right for me as president of the United States to be visiting Kenya when those issues need to be worked on,” Obama said.

But the US leader said he had visited Kenya multiple times before he was president and expected to return.

“My personal ties to the people of Kenya, by definition are going to be strong and will stay strong,” he said.

Obama’s Africa tour started in Senegal, and he is currently in South Africa. He will wrap up his week-long journey in Tanzania.

Source: Capital fm 

GHASIA ZAIDI MISRI


Watu wawili mmoja wao akiwa na asili ya Kimarekani wameuwawa wakati waandamanaji walipovamia ofisi ya chama tawala nchini Misri cha Muslim Brotherhood, Udugu wa Kiislamu mjini Alexandria. 

Hii imeongeza wasiwasi mkubwa  maandamano yaliopangwa kufanyika hapo kesho(30.06.2013)yanayonuiwa kumng’oa madarakani rais Mohammed Mursi baada ya mwaka mmoja tangu kuwapo  madarakani.
Maafisa nchini humo wamesema Mmarekani huyo aliye na umri wa miaka 21aliyekuwa akifanya katika shirika la kitalii la Marekani lililoko mjini Alexandria aliuwawa alipokuwa anachukua picha za waandamanaji.
Wakati huo huo mtu wa tatu mwengine ambaye ni muandishi  habari  raia wa Misri, aliuwawa na wengine walijeruhiwa katika shambulizi la bomu kwenye maandamano mengine mjini Port Said. Polisi nchini Misri inasema chanzo cha shambulizi hilo hadi  bado hakijajulikana ingawa waandamanaji wanaamini ni bomu lililolengwa katika afisi ya chama cha Waislamu walio na itikadi kali.
Hata hivyo  viongozi  maarufu  wa  kidini  nchini Misri wameonya juu ya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe hasa baada ya ghasia za wiki iliopita ambako watu kadhaa waliuwawa na wengine walijeruhiwa.  Viongozi  hao wameunga mkono hatua ya rais Mursi ya kutaka kuzungumza na upinzani kabla ya kufanyika maandamano makubwa hapo kesho.
Mohammed Mursi atimiza mwaka mmoja madarakani
Rais wa Misri Mohammed Mursi aliye na umri wa miaka 62 na aliyechaguliwa kwa njia ya kidemokrasia kuongoza   hapo kesho anatimiza mwaka mmoja tangu alipoanza kazi.
Sasa baadhi ya raia anaowaongoza wanamtaka aondoke madarakani kwa madai kuwa ameshindwa kutimiza matakwa ya waandamanaji mwaka 2011 waliomuweka madarakani na pia kutowashughulikia wapiga kura wengine milioni 50 ambao hawakumchagua mwaka uliopita.
Maandamano ya hapo kesho yameitishwa na  la Tamarod vuguvugu ambalo linadai kuwa na saini milioni 15 za watu wanaomtaka rais Mursi kuondoka madarakani na kuitisha uchaguzi wa haraka.
Waandamanaji wamesema haja yao sio kumtoa Mursi madarakani peke yake lakini ni kwa yeyote ambaye hatatimiza matakwa yao ya chakula, amani, haki ya kijamii na haki ya kibinaadamu.
Kwa upande wake kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood Mohamed al-Beltagui amesema hawatakubali kamwe mapinduzi dhidi ya Rais Mursi.
Amnesty International yatoa tamko
Msemaji wa afisi ya rais wa Marekani Patrick Ventrell amesema Marekani inaomba pande zote mbili kuwa watulivu. Ventrell amesema viongozi wa kisiasa nchini humo wana wajibu wa kuhakikisha kuwa ghasia hazitokei nchini humo.
Hata hivyo jana jioni Marekani imesema raia wake pamoja na wanadiplomasia wanaweza kuanza kuondoka Misri kwa sababu za kiusalama.
Kwa upande wake Ujerumani imemtaka rais Mohammed Mursi kufanya mabadiliko ya haraka ili kuzuia umwagikaji wa damu zaidi.
Tangu kuanza kwa ghasia wiki iliopita nchini Misri watu watano tayari wameuwawa huku wengine wengi wakiwa  wamejeruhiwa. Shirika la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limetaka vikosi vya serikali kuhakikisha kuwa hawatumii nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji na kuhakikisha maandamano yanafanyika kwa amani.
Hassiba Hadj Sahraoui naibu mkurugenzi wa shirika hilo katika Mashariki ya kati amesema ni lazima utawala uweke wazi kuwa mtu yoyote atakayeonekana kutumia nguvu kupita kiasi atakabiliwa na mkono wa sheria.
Wakati huo huo jeshi lililoshuhudia kipindi cha mpito kutoka kwa utawala wa Mubarak hadi ule wa Mursi limeonya kuingilia kati iwapo ghasia zaidi zitashuhudiwa.

MAMIA NCHINI AFRIKA KUSINI WAJITOKEZA KATIKA MAANDAMANO YA AMANI YA KUPINGA KUJA KWA RAISI OBAMA



 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini wakiwa wamebeba mabango yanayopinga kuja Kwa Raisi Obama nchini Humo wakati wa maandamano ya Amani ya Kupinga Kuja Kwa Obama Katika Jiji la Pretoria Nchini Afrika  jana Jioni - Juni 28

 Waandamanaji Nchini Afrika Kusini Wakisali mbele ya Bango linalopinga Kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo wakati Raisi Obama alipotua Nchini Afrika Kusini Jioni ya jana  Juni 28

 Waandamaji wa Nchini Afrika Kusini wakiwa wanasali mbele ya Ubalozi wa Marekani wakati wa maandamano ya kupinga kuja kwa Raisi Obama Nchini Humo jana  wakati Raisi Obama alipotua Nchini Humo Kwa Ziara ya Siku 2 ..

Mmoja wa waandamaji nchini Afrika Kusini ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akiwa amebeba moja ya Bango ambalo Linamwita Raisi OBAMA kuwa ni Mpishi wa Ikulu ya Marekani kama linavyosomekana na kuendelea kuelezea kuwa sera za Marekani ni tatizo.Mwandamaji huyu alibeba bango hilo jana  Juni 28 wakati wa maandamo ya amani kuelekea mbele ya Ubalozi wa Marekani NChini humo kwa kupinga Kuja Kwa OBAMA Nchini Mwao.Picha Zote na REUTERS/AFP

Friday 28 June 2013

Kaseja atetewa


Kaseja 

  • Wadau wengi wanataka Simba ibadilishe uamuzi wa kumtema Juma Kaseja kwa vile bado ana uwezo mkubwa na ndiyo maana ni nahodha wa Taifa Stars.

Dar es Salaam.  Baadhi ya wadau wa soka, wamekosoa uamuzi wa klabu ya Simba kutangaza kumtema kipa wake namba moja, Juma Kaseja na kusema hatua hiyo imechangiwa na siasa za chuki dhidi ya kipa huyo.
Kwa wiki nzima sasa, suala la Kaseje kutemwa limekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari, huku ikielezwa kuwa uamuzi huo umewagawa viongozi wa klabu, kwani baadhi yao wanataka aendelee kubaki.
Rafiki wa karibu wa Kaseje amelitonya gazeti hili jana kuwa, kipa huyo kwa sasa yuko nje ya jiji na kwamba anatarajia kuzungumza kwa mara ya kwanza kuhusu hatima yake Simba Jumapili wiki hii.
Mwenyekiti wa Simba na hata kocha Abdallah Kibadeni walikaririwa wakisema, kipa huyo aliyesajiliwa mwaka 2003 kutoka Moro United hatakuwamo kwenye kikosi hicho msimu ujao.
Kipa wa zamani wa klabu hiyo, Moses Mkandawile ameshutumu uamuzi wa Simba kumtema Kaseja kwani, yeye binafsi anaamini Kaseja ndiye kipa bora kwa sasa Tanzania.
“Huyu ni nahodha wa timu ya Taifa, ikiwa na maana kwamba kiwango chake bado kiko juu. Sasa iweje Simba wamteme kwa madai ya kushuka kiwango? Kweli uamuzi huu unashangaza sana,” alisema Mkandawile.
“Nadhani kuna chuki binafsi kati yake na baadhi ya viongozi ndiyo maana wengine wanapinga Kaseja kutemwa,” alisema zaidi kipa huyo wa zamani.
Aidha, Katibu Mkuu wa zamani TFF, Fred Mwakalebela naye alishangazwa na uamuzi wa Simba kumtema kipa huyo na kusema haukuzingatia uwezo wake, bali chuki kutoka kwa baadhi ya viongozi wake.
Mwakalebela alisema, anaamini Kaseja bado ni kipa mwenye uwezo wa kucheza timu yoyote kwa vile kiwango chake bado kinadai tofauti na mawazo ya watu wengine.
Kwa upande wake, mchezaji wa zamani Yanga  Kitwana Manara alisema walichokifanya kwa Kaseja siyo sahihi hata kama mpira umekwisha anatakiwa apewe heshima yake kama mchezaji aliyeitumikia klabu muda mrefu.
“Huyu ni alama ya mafanikio Simba, alipaswa kupewa heshima kubwa. Kama hawataki kumsajili, basi wangemweka kwenye benchi la ufundi,” alisema Manara.
Kwa upande wake, nyota wa zamani Taifa Stars, Peter Tino alisema masuala ya usajili waachiwe viongozi na benchi la ufundi na kwamba wasisikilize kelele za mashabiki.

BINTI AJIFUNGUA BARABARANI MOROGORO

 PICHA NA HABARI SOMA HAPA


Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.
 
Tukio hilo lililo

washtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.

Mwandishi wetu alifika eneo la tukio na kumshuhudia askari wa kike wa kikosi cha usalama barabarani ‘trafiki’ (jina lake halikupatikana) akiacha kazi ya kuong
oza magari na kugeuka mkunga kwa muda ili kumsaidia binti huyo akiwa sambamba na wanawake wengine na kufanikisha kupatikana kwa mtoto wa kiume ‘dume la nguvu’.
Mmoja wa akina mama waliofika eneo hilo akiwa amembeba mtoto wakati mama yake akihojiwa na mwanahabari.
Awali, wanawake hao walizungusha kanga ili kuweza kuweka usiri wakati wa kumsaidia mwanamke mwenzao alipokuwa akijifungua.

Mara baada ya zoezi hilo kwenda salama, Josephine alisema alipatwa na uchungu alfajiri ya siku hiyo na mume wake aliwapigia simu madereva wa teksi zaidi ya wawili ambao waligoma kufika kijijini kwao kutokana na ubovu wa barabara.


Kulia ni trafiki aliyemsaidi Josephine kujifungua na kushoto mtoto aliyezaliwa akiwa amebebwa.
“Hali ilipozidi kuwa mbaya tuliwasiliana na dereva wa bodaboda ambaye alifika na kunibeba huku mume wangu akitufuatilia nyuma kwa baiskeli yake,” alisema Josephine kwa uchangamfu.

Binti huyo alisema kwamba walipofika eneo la Nanenane hali ilizidi kuwa mbaya akashindwa kujizuia baada ya mtoto kushuka chini, hivyo akamuomba dereva wa bodaboda asimame ndipo alipoanguka chini na hali kuzidi kuwa mbaya.


Wananchi waliofika eneo hilo wakiwa na Josephine (aliyekaa chini).
Baada ya kuliona tukio hilo, trafiki na wanawake wengine waliokuwa jirani wakajitolea kumsaidia hadi alipojifungua salama.
Dereva wa bodaboda aliyembeba Josephine anayejulikana kwa jina la Gitogo Shilagi alikiri barabara iendayo Kijiji cha Kiegea kuwa mbovu.

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya Josephine kujifungua salama mtoto wa kiume.
source: Juma mtanda blog


Kiongozi mkuu wa Al Shabaab ajisalimisha



sheikh-hassan-dahir-aweysUmoja wa mataifa unasema kuwa kiongozi mmoja mkuu wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia, al-Shabab, Hassan Dahir Aweyes, amejisalimisha kwa wanajeshi wa Somalia.
Bwana Aweyes alitafuta hifadhi mjini Adado,mji ulio umbali wa kilomita miatano kaskazini mwa Mogadishu baada ya mapigano makali kati ya mirengo ya Al Shabaab mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa kiukoo, wamekwenda huko kujadili watakachofanya naye baada ya kujisalimisha kwake.
Lakini viongozi hao wamefahamisha mwandishi wa BBC kuwa amekanusha madai kuwa amejisalimisha na kwamba amekataa kusafiri kwenda Mogadishu.
Bwana Aweyes amekuwa akijulikana kama kiongozi mkubwa katika kundi la al-Shabab na Umoja wa mataifa na Marekani zinamfahamu kama gaidi


Wakesha wakimuombea Mzee Mandela



Mandela bado anaugua sana hospitalini
Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.
Wakati huohuo mwanawe Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.
Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto
"leo angalau yuko sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD RAIS OBAMA



Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.

Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.

Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor.

VIDEO YA WEMA SEPETU AKIWAPOROMOSHEA MATUSI MAZITO WAFANYAKAZI WAKE WA NDANI



STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi.  

Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.  

Ilikuwa majira ya asubuhi ambapo Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006/07, akiwa ametinga dela, nywele bandia nyekundu na miwani nyeusi, alikuwa amejiandaa kwa ajili ya mtoko lakini alipoingia kwenye gari lake aina ya Toyota Lexus Harrier ndipo akagundua tatizo. 

Cha kwanza alichogundua ni kwamba gari hilo lilikuwa limeibiwa power window (mashine ya kushusha na kupandisha kioo) zote.

Cha pili ni kwamba alipopiga ‘stati’ gari hilo lilikataa kuwaka kutokana na kuchokonolewa kwenye betri.

Baada ya kuona hivyo, Wema aliwaita wafanyakazi wake wawili, mmoja wa kiume na mlinzi na kuanza kuwawashia moto kuwa walikuwa wakijua kilichoendelea.  

Wema alianza kuwahoji kuwa walilifanya nini gari hilo, waliponyamaza kumjibu ndipo akapandwa na hasira na kuanza kutoa mkong’oto kwa kutumia chochote alichokutana nacho mbele yake.

  Huku akimmwagia maji machafu yule mlinzi wa kiume na kumpiga kwa dekio la plastiki, Wema alikuwa akimwaga mitusi mizito ya nguoni isiyoandikika  kutokana na ukali wake. 

  “My friend ninyi ni mabogasi kabisa, nawaambia mtaozea Segerea, mnafanya nini hapa ninyi wa…(tusi) au mna…(tusi kali). 


 “Ninyi ni …(tusi kubwa likihusisha mama zao), mnakaakaa tu hapa wa…(tusi tena), mnajua bei ya power window? Mnadhani hili ni Toyota? Kwa taarifa yenu hili ni Lexus …(tusi) zenu,” alisikika Wema akitumia lugha ya matusi ambayo asilimia kubwa hayaandikiki kwa namna yoyote kutokana na kupitiliza.

Wema aliendelea kuwakimbiza ndani ya fensi akiwapiga huku sauti ya Martin Kadinda (yule meneja wake) ikisikika, ‘Mwache ataruka ukuta, nenda karipoti polisi’.

  Huku akiwa mbogo, Wema alimgeukia mmoja wa mbwa wake aitwaye Fiona na kumuwashia moto huku akimmwagia mitusi:

“Na wewe Fiona unakaa hapo hapo unamuuzia nani sura badala ya kulinda mlinzi, sipendi mambo ya ki… (tusi)

Mkurugenzi huyo wa kampuni ya kufyatua filamu ya Endless Fame Production alikwenda mbali na kuwatuhumu wafanyakazi hao kuwa kuna uwezekano wanatumiwa kumhujumu akiahidi kuwakomesha.

“Mnatumwa mnapewa pesa ili mnifanyie hivi…gari litaibiwaje power window likiwa ndani na ninyi mkiwepo? Wa…(tusi) sana ninyi,” alisikika msanii huyo.  

Katika hali ya kushangaza, badala ya kumuwashia moto mlinzi anayehusika na usalama nyumbani hapo, Wema ‘alidili’ na wafanyakazi wa ndani tu huku mlinzi naye akishindwa kumuamulia na kubaki kumtazama tu namna alivyokuwa akikimbizana na wafanyakazi hao.

 Kwa upande wao majirani walikuwa wakila chabo na kusikitishwa na mvua ya matusi aliyokuwa akiitoa msanii huyo ambaye ni kioo cha jamii.

  “Jamani jamani, hivi hajui tuna watoto wadogo ambao hawastahili kusikia matusi makubwa kama anayomwaga? “

Ukweli Wema anatusikitisha sana kwa sababu watoto wanajifunza nini kutoka kwake?” alihoji mmoja wa majirani hao aliyeomba hifadhi ya jina ili na yeye asije akawashiwa moto na msanii huyo.

source:GPL:

GARI LA KUBEBA MAFUTA LAANGUKA KIBAHA

 WATU KAMA KAWAIDA NA VIDUMU VYAO


2093648 orig 8c4d3
7076096 orig aa465Lori moja la kubebea  mafuta ya vyombo vya moto likiwa limeanguka eneo la Kongowe, Kibaha kama lilivyokutwa na mpiga picha jioni ya leo. Wananchi wanaonekana wamelizungukaa   hawanahofu ya hatari inayoweza kutokea kama zilivyotokea nyingine siku zilizopita

Thursday 27 June 2013

VIDEO YA OBAMA AKIWASILI SENEGAL

Pichani ni rais OBAMA wakati akiwasili nchini Senegal leo mapema

HAWA NDIO MASTAR WA KIKE WAKALI SANA BONGO!!


  sintah/ blogger, actress 
Wema Sepetu (actr ess/former miss Tanzania)

Bridgitte Alfred (Miss Tanzania 2012)Tunakubariki miss tanzania

Millen Magese (former miss Tanzania)

Jokate Mwegelo (presenter/fashion designer)KIDOTI

Teddy Kalonga (model)

Mange Kimambi (creative director)muke ya muzungu..

Penny Mungilwa (Mtangazaji)muke ya mwanamuziki mukubwa bongo..
Jackline Ntuyabaliwe (Former Miss Tanzania)

Vanessa Mdee (Mtangazaji/Msanii)

Salma Msangi (Mtangazaji)

Jackie Cliff (model)alekizanda makwinii, BOSS LADYY(NANI KANUNA???

Hamisa anguwh (model) dada mlezi ahahahahhhh

So guys katika hii list dah!! Pongezi za dhati kabisa ziwaendeee kamati ya Miss Tanzania kwa kuibua watoto wakali ambao wanatikisa zaidi Bongo, mdau wangu we unaonaje kwani?? Tumepatia au tumebuma?? Nani kakosekana hapa kwenye listi ulitaka awekwe au mwingine kaekwa unataka atolewe?

Ufupi wa kaptura ya binti wa Obama wazua gumzo


malia-obama-short-shorts-0Binti mdogo wa rais Barack Obama, Sasha, alikua jijini New York hivi karibuni akifanya shopping huku amevaa kikaptura kifupi (short shorts, al maarufu kama daisy dukes.) Mapaparazzi walimpiga picha binti huyo akiwa mitaani na raha zake na kuuliza mitandaoni kama ni sahihi kwa binti wa miaka 12, kuvaa kaptura fupi hivyo. Kama kawaida za mitandaoni, kilichozuka ni ubishi mkali kati ya wanaoona si sahihi, hasa kwa binti ya rais, na wale wanaoona ni poa tu. Wewe upo kwenye camp ipi? Unaweza ruhusu binti yako avae kaptura kama hii? malia-obama-short-shorts-0
malia-obama-short-shorts
malia-obama-short-shorts-1

ANUSURIKA KUNYONGWA NA MUME WAKE AMBAYE NI POLISI MKOANI IRINGA.


Hapa Rehema akiwa wodini katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa alipokimbizwa kwa matibabu kutokana na kipigo kikali toka kwa askari huyo, ambaye ni mume wake.Haya ni baadhi ya majeraha ambayo aliyapata shingoni kutokana na kukabwa shingo na askari huyo.

Bi Rehema akiwa nyumbani kwa wazazi wake baada ya kukimbia nyumba yake kutokana na kipigo kisichokwisha 
Mama mzazi wa Rehema akiwa Monica Shauri
 
Rehema Shauri Madongo ni mmoja kati ya mwanamke ambaye amebahatika kuolewa na askari polisi kitendo cha upelelezi ambaye anaeleza jinsi alivyotendewa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuteswa na kupigwa kikatili na pindi anapofika polisi hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye ni askari .

 Kwa alisema toka ameolewa kila mara amekuwa akipokea kipigo na mbaya zaidi kabla ya kupigwa amekuwa akifungwa mikono kwa pingu zinazotumika kuwafunga watuhumiwa pingu ambazo mume wake huyo amekuwa akizihifadhi ndani ya nyumba. 
" Kweli inasikitisha sana kusimulia kwani kabla ya kupigwa nimekuwa nikifungwa pingu mikono kama mharifu sugu na baada ya hapo kipigo kikali kimekuwa kikinikuta ....hadi sasa nimepigwa zaidi ya mara 20 na polisi nimekwenda kuripoti mara tatu na Hospital nimelazwa mara moja ila siku nyingine nimekuwa nikiugulia nyumbani ila nyumbani kwa wazazi nimerudi mara tatu sasa"
Alisema kuwa mbali ya kupigwa na kuumizwa ila kuna mateso mengine ambayo amekuwa akiyapata kutoka kwa mwanaume huyo ni siri yake na hayapaswi kuelezwa hapa kutokana na jinsi ambavyo askari huyo anavyomtenda ukatili wa kinyama. Hata hivyo alisema kuwa akiwa na mimba ya mwezi mmoja hali ya kipigo ilizidi zaidi na wakati mwingine alipata kumfunga shingo na kanga kwa kutaka kunyonga shingo huku akitishi kumuua
Aidha alisema kuwa kila akifika polisi kufungua kesi hakuna utekelezaji unaofanyika kutokana na polisi kulindana  kwa suala hilo. Pia alisema mbali ya kupigwa akiwa nyumbani kwake ila bado anapoamua kukimbia nyumba hiyo na kukimbilia kwa wazazi wake bado askari huyo amekuwa akimfuata na kumpa kipigo mbele ya wazazi wake, tendo ambalo limempelekea yeye na Mama yake
wamekuwa wakiishi ndani wamejifungia milango kuogopa askari huyo kuja kuwafanyia ukatili, ikiwa ni pamoja na kuwaua kwa risasi kama ambavyo amekuwa akiwatisha mara kwa mara.
Bi Shauri alisema mbali ya kuwa yeye ni mmoja wa wacha Mungu kwa maana na Mlokole mzuri ambae kila wakati asubuhi lazima aende kusali ila kwa sasa anaogopa kutoka asubuhi kwa kuhofia kuvamiwa na askari huyo . Hivyo aliomba jeshi la polisi kuweza kumpa ulinzi yeye na familia yake ama kumkamata mtuhumiwa huyo ambae inadaiwa kwa sasa yupo katika mji wa Iringa. 

Miaka minne baada ya kufariki kwa King of Pop Michael Jackson (June 25), Hii ndiyo hali iliyokutwa kaburini kwake


Moja ya shabiki wa ukweli aki-show love