RIPOTI MAALUMU KUHUSU VURUGU ZILIZOTOKEA JANA BUNGENI.
Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle),
unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka
alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo,
Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine
kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake.
Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya
Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anadaiwa kumpiga kichwa Askari
wa Bunge na kumchania sare na kung’oa kipaza sauti.
No comments:
Post a Comment