Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda muda huu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro.
Sheikh Ponda amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali akisindikizwa na msafara wa magari yaliyokuwa na polisi.
Ponda amesafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam mpaka mkoani Morogogro kwa usafiri wa helkopta iliyotua katika viwanja vya Gymkhana.
No comments:
Post a Comment